Thursday 20 August 2015

INNOCENT MELLECK SHIRIMA ACHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA VUNJO.

Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Vunjo,Innocent Shirima akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kufika ofisi za msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi.
Mgombea Ubunge jimbo la Vunjo ,Innocent Shirima akikabidhiwa fomu za kuwania ubunge katika jimbo la hilo na msiamizi wa Uchaguzi ,Furgence Mponji ambaye pia ni mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Mgombra Ubunge wa jimbo la unjo kupitia chama cha Mapinduzi,Innocent Shirima akionesha fomu zake za kuwania Ubunge katika jimbo hilo.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo,Innocent Shrima akiwa na makada waliomsindikiza wakatialipofika ofisi za msimamizi wa uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Knada ya Kaskazini.

MAGUFULI ASAINI HATI YA KIAPO YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAKAMA KUU JIJINI DAR LEO.

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli  akikabidhi hati ya Kiapo mapema leo mchana kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Sekieti Kihiyo (katikati). Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
 Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli akisaini hati ya Kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
 Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Jaji Sekieti Kihiyo mara baada ya  kusaini hati ya kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa ndani ya moja ya chumba cha Mahakama Kuu wakirekodi tukio la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli sambamba na mgombea Mwenza,Samia Suluhu Hassan walipokuwa wakisaini hati ya Kiapo mapema leo mchama Mahakamani Hapo mbele ya Jaji  Sekieti Kihiyo. 
 Mgombea urais wa chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nje ya jengo la Mahakama Kuu mara baada ya kusaini hati ya Kiapo mapema leo mchana.Hati hiyo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.

JAMES MBATIA AKABIDHI ZAWADI KWA BINGWA WA MASHINDANO YA JIMBO LA VUNJO (MBATIA CUP 2015).

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia akiwasili katika uwanja wa Himo Polisi kwa ajili ya kushuhudia fainali ya Mashindano ya Kombe la Jimbo ,maarufu kama Mbatia Cup 2015.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi taifa,James Mbatia akisamiana na wachezaji wa timu ya Wazalendo fc kabla ya kuanza kwa mchezo.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia akikagua kikosi cha wachezaji wa timu ya Himo fc.
Kikosi cha timu ya Himo fc.

MGOMBEA URAIS WA CHADEMA, EDWARD LOWASSA NA MWENZA WAKE DUNI HAJI, WASAINI HATI YA KIAPO

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisaini fomu za
hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania,
Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Hati ambayo kila mgombea wa
nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es
Salaam ili kuthibitisha usahihi wa fomu hizo kabla ya mkuzirejesha Tume
ya Taifa ya Uchaguzi, kwa uteuzi. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Juma Haji
Duni, maarufu kama “Babu Duni”
 
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni
akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
hicho, Mh. Edward Lowassa.
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza
wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu (mbele) wakati wa kusaini fomu za hati
ya Kiapo, leo Agosti 19, 2015. Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh.
Mabele Marando.
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za
hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman
Said Komu.
 
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni
akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania,
Jaji Suleiman Said Komu. Kulia ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.
 

RAIS KIKWETE AMTAMBULISHA MGOMBEA URAIS NA MGOMBEA MWENZA WA CCM KWA WAZEE WA DAR ES SALAAM


1
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Mgombea mwenza wa ugombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho tawala Dkt John Pombe Magufuli leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
PICHA NA IKULU
2
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam 
leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
3
Meza Kuu ikimfurahia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
4
7
5
Mwenyekiti wa Wazee wa CCM wa Dar es salaam akipeana mikono na Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuongea na wazee wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
6