Sunday, 28 September 2014

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KATIKA JIMBO LA MLALO WILAYANI LUSHOTO


1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kwekangaga ambapo alishiriki kazi ya ujenzi wa ofisi ya CCM ya tawi hilo na kuongea na wananchi, Kinana yuko mkoani Tanga akihimiza na kukagua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ambapo leo amefanya ziara yake katika jimbo la Mlalo linaloongozwa na mbunge Brigedia Jenerari Hassan Ngwilizi, Katika ziara hiyo pia  anaimarisha  uhai wa chama akiwa ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MLALO-LUSHOTO)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisomewa taarifa na mmoja wa viongozi wa kijiji hicho ambaye katika taarifa yake ya ujenzi wa ofisi hiyo baada ya kusoma taarifa iliyokuwa ikielezea gharama kubwa za ujenzi wa ofisi hiyo ilitajwa kufikia  milioni 45.000.000 wakati thamani halisi ya ujenzi wa jengo hilo ni milioni 4.500.00001Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Kwekangaga kulia anayempatia tofali ni mwenyekiti wa CCM wilaya  ya Lushoto Mzee Mshangama2Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya wakiwa katika kikao cha ndani na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe hao katika mkutano wa ndani uliofanyika kwenye kata ya Lukozi.
8Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Sunga Mlalo10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Sunga Mlalo.11Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga akijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Sunga jimbo la Mlalo12Mmoja wa wananchi akiuliza swali wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliporuhusu wananchi hao kuuliza maswali katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika Sunga jimbo la Mlalo.13Mwandishi wa habari Hosea Cheyo wa TBC akichmrekodi mmoja wa wananchi waliokuwa wakiuliza maswali katika mkutano huo.14Kikundi cha K Square Comedy kikiwachekesha wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.16Katika Mkutano huo pia wageni kadhaa kutoka nje wamehudhuria.

No comments:

Post a Comment