Wednesday, 17 September 2014

SAFARI YA KINANA KUTOKA NYAMISATI MPAKA MAFIA KWA BOTI YA KIZAMANI

16 
Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jamno pamoja na wabunge wa Mafia Abdulhimid Shah kulia na Abdull Marombwa wakati Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnnauye alipokuwa akiwaaga wananchi katika mji wa Nyamisati wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ukielekea Mafia wakati akiwa katikaziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo. 12 
Boti ikikata mawimbi baharini huku bendera za CCM zikipepea. 18 
Mawimbi makali kidogo lakini ndiyo mwendo wenyewe. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitoa burudani mara baada ya kwasili kisiwani Mafia jana. 28 
Naibu Waziri wa Nishati nishati na madini Mh. Charles Kitwanga akiwahutubia wananchi wa Mafia na kuwaelezea mipango ya serikali juu ya huduma ya umeme katika kisiwa hicho.

No comments:

Post a Comment