Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman
Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo
asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano
Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima
bila kikomo.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa
Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la
Polisi mapema leo.
Baadhi ya wapenzi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), wakishangilia baada ya gari lililokuwa limembeba Mwenyekiti
wa chama hicho, Freeman Mbowe, alipowasili leo Makao Makuu wa Jeshi la
Polisi jijini Dar es Salaam, kwa mahojiano.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na waandishi wa
habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya
kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa
Chama hicho na Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila akihojiwa na askari
Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa
kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
alihojiwa na Polisi.





No comments:
Post a Comment