Saturday, 25 October 2014

Mwandosya amuwakilisha JK Sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Zambia

unnamed
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya  akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo. unnamed3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya (wa tatu kulia ) pamoja na Mkewe Lucy Mwandosya wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa wa Zambia wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Wengine kutoka kulia ni Kaimu Rais wa Zambia Mhe Edgar Lungu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, na wa  pili kulia ni Makamu wa Rais wa Nigeria Monance Namadi Sambo. unnamed5 

No comments:

Post a Comment