Monday, 24 November 2014

CCM YASONGA MBELE KWA KUTEKELEZA ILANI YAKE NA KUHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya kijiji cha Marika jimbo la Lulindi wakati akiwa katika ziara jimboni humo akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali na kuhimiza uhai wa chama katika jimbo hilo lililop0 wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Katika ziara hiyo ya mikoa ya Lindi na Mtwara Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikasi, Siasa na Uenezi. Kesho Kinana anaendelea na ziara katika wilaya ya Newala.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-LULINDI -MASASI)2 
Mtambo wa kuchimbia mifereji ukiendelea na kazi ya kutengeneza tuta la bwawa hilo katika kijiji cha Marika.4 
Akina mama mbalimbali wakimpokea Katibu Mkuu Kinana wakati alipowasili katika mradi huo.5 
Afisa CCM makao makuu Lumumba Bi. Gift Msuya akikitunza kikundi cha kwaya cha Chiungutwa wakati kilipokuwa kikitumbuiza katika mkutano huo.13 
Mbunge wa jimbo la Lulindi Mh. Jerome Bwanausi akizungumza na wananchi katika mkutano huo.14 
Baadhi ya kadi zilizorejeshwa na wanachama wa vyama mbalimbali Chiungutwa na kujiunga na CCM.16 
 17 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaongoza wanachama wapya kula kiapo cha utii kwa chama kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe.

No comments:

Post a Comment