Tuesday, 25 November 2014

KINANA ATEMBELEA DARAJA LA UMOJA MTAMBASWALA NA KUSHIRIKI SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO

2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiponda mawe wakati aliposhiriki katika ujenzi wa Bwawa la maji lilalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo leo Kinana amefanya kazi mbalimbali pamoja na kufanya mikutano kadhaa akiwa ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NANYUMBU-MTWARA)3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na mafundi kupanga mawe katika ukingo wa bwawa hilo linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mganga Mfawidhi  wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo wakati alipokuwa akikagua kituo cha afya cha Mangaka wilayani Nanyumbu ambapo ameelezwa kwamba kituo hicho kimeomba kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya ambapo kimekidhi vigezo vyote lakini wamesubiri kwa miaka mitatu bila mafanikio.5Mganga Mfawidhi  wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo  akizungumza na waandishi wa habari adha wanayoipata wagonjwa kutokana na kutopandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya pamoja na kukidhi vigezo vyote vya kuwa hospitali ya wilaya.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo katika chumba cha upasuaji kutoka kwa Mganga Mfawidhi  wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mganga Mfawidhi  wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo mara baada ya kutembelea kituo hicho katikati ni Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo S. Kiswaga.8Kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la Umoja10Ni Daraja lenye urefu wa zaidi ya mita 700.11Kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani, Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la Umoja

No comments:

Post a Comment