Na Mahmoud Ahmad, Arusha
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ,(Uhusiano na Uratibu ) , Stephen Wasira amesema kuwa yupo tayari kuvunja makundi ya kudumu yanayoongozwa na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Felix Mrema pamoja na Batilda Burian aliyekuwa mgombe wa ubunge na kushindwa kwa chama hicho kwenye chaguzi mbali mbali.
Aidha amesema kuwa Arusha inashindwa kwenye chaguzi mbalimbali kutokana na makundi yaliyopo ndani ya chama hicho na si kwasababu ya vyama vya upinzani kuwa na nguvu ya kuiangusha CCM.
Wasira aliyasema hayo jana Jijini hapa kwenye kikao cha Halmashauri ya Wilaya kilichofanyika jana ndani ya ukumbi wa CCM Mkoa na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa chama hicho chenye lengo la kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za wenyeviti wa mitaa.
Alisema makundi ya Batilda na Mrema ni lazima yamalizwe na kama mlezi yupo tayari kuyaita makundi hayo ili kumaliza tofauti zilizopo ndani ya chama na kutoa rai kwa wagombea wengine kuwa kama wameshindwa wakubali kushindwa na kumpa ushirikiano mgombe aliyepitishwa kwa wakati huo ila si vyema kuweka makundi ndani ya chama.
“Nakerwa sana na kushindwa kwetu kwenye chaguzi ambao sisi wenyewe ndio tunaofanya tushindwe na kwanini tunaendelea kushindwa kwenye chaguzi mbalimbali sisi tukishinda au kushindwa tunapongezana hili ni tatizo hata kama tumeshindwa tunapongezana haiwezekani lazima tufike mahali tuvunje makundi na kuchagua kiongozi/mgombea aliyemteule na si kuongozi asiyetakiwa na wananchi”.
Hata kamati za Siasa Mkoa wa Arusha nazo pia zimegawanyika waandika maazimio na kamati nyinge zinakaa na kuyakataa hapana tunachane na makundi na pia tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa lazima tuchague kiongozi mteule na si kumchagua mjomba wala shangazi yako maana akishindwa tunashindwa wote kama chama na si wewe uliyetaka awepo.
Alihoji suala la wananchi wa Kijiji cha Nanja kilichopo Wilayani Monduli kuandamana hadi Ofisi za Mkoa kutoa malalamiko yao kuwa mgombea waliyemtaka si yule aliyepitishwa na kutoa tahadhari kwa wananachama na viongozi kuwa kwanini wanataka kuwa wabinafsi na kuhoji kwanini mteule asipitishwe badala yake apitishwe mgombea asiyetakiwa na wananchi wa eneo husika/.
Aliongeza asijidanganye mtu Rais ajaye atatoka ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwani hata maandiko yanasema kuwa wagombea ni wengi lakini wateule ni wachache .
Pia Wassira aliwasihi wanachama wa CCM pamoja na wananchi kwa ujumla kujitokeza kupiga kura ya maoni kwaajili ya katiba mpya pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kutimiza wajibu wao.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, onesmo ole Nangole awali akikaribisha Wassira ambaye ni mlezi wa chama hicho Mkoani hapa alisema kuwa kinachokiangusha CCM kwenye chaguzi mbalimbali Mkoani hapa ni makundi ndani ya chama na kuyataja makundi hayo kuwa yanaongozwa na Batilda pamoja na Mrema huku akimsihi Wassira kuwaita kwa pamoja na kuwafungia ndani ili waweze kujadili kiini cha makundi hayo na kuyavunja kabisa.
Nangole alihoji ni kwanini wanaangusha wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama na kutoa rai kwa wanaccm kuachana na majungu na kuacha watu kuamua nani wanayemtaka badala yake wasipeleke wateule mizigo kwenye chaguzi halafu mwisho wa siku chama kinashindwa kwenye chaguzi mbalimbali.uchaguzi unapofika tuweke nia ya kushindwa na kupongezena

No comments:
Post a Comment