Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo
aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya
Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya
makundi hasimu.
Baada
ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya
kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo
Kutoka
kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa
Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo
Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha.
Viongozi
wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa
kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha
SPLM.
Hapa
wakiwa na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti, na yakiwa
yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu
Ndugu Abdulrahman Kinana.


No comments:
Post a Comment