Thursday, 29 January 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AZURU KABURI LA ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS HAYATI DR.OMAR ALI JUMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wageni wakati alipozuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais Hayati Dr. Omar Ali Juma aliyefariki mwaka 2001 katika kijiji cha cha Wawi Mchekeni wilaya ya Chakechako mkoa wa Kusini Pemba leo, katikati ni MNEC wa wilaya ya Chakechake Bw. Daud Ismail.(PICHA NA KIKOSIKAZI FULLSHANGWE- KUSINI PEMBA)
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wakiomba dua wakati Katibu Mkuu huyo na msafara wake walipozuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais Hayati Dr. Omar Ali Juma.
 Baadhi ya viongozi wanawake nao wakijumuika kuomba dua.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa kahawa na baadhi ya viongozi kutoka kulia ni Balozi Ali Karume mjumbe wa halmashari kuu ya Taifa, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai  na Mzee Ali Abdalla Ali.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakichimba msingi wakati aliposhiriki ujenzi wa madarasa katika skuli ya msingi ya Tumbi Chambaageni wilaya ya Mkoani.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akishiriki ujenzi wa madarasa katika skuli ya msingi ya Tumbi Chumbaageni wilaya ya Mkoani Kusini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakipanda mbogamboga wakati alipotembelea na kukagua shughuli za kilimo cha mbogamboga zinazofanwa na kikundi cha ujasiriamali cha Jambo Group Corporation Society chenye wanachama 15 katika Shehia ya Wambaa kwa Anzani kulia ni Hafidh Ali Juma Katibu wa kikundi hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua kilimo cha mbogamboga la kikundi cha Jambo Group Corporation Society kushoto ni Hafidh Juma Ali Katibu wa kikundi hicho.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutka kwa Hafidh Juma Ali katibu wa kikundi cha Jambo Group Corporation Society alipokitembelea kikundi hicho Wambaa kwa Anzania.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na viongozi wengine akirejea mara baada ya kukagua kilimo cha mbogamboga katika kikundi cha Jambo Group Corporation Society
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa tawi la CCM la Milimuni wilaya ya Mkoani Kusini Pemba.
 Shamba la migomba la kikundi cha Utandawazi Corporation Group Society kinachojisughulisha na kilimo cha ndizi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda migomba katika shamba la kikundi cha Utandawazi Corporation Group Society.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana CCM wakati alipomtembelea balozi Ame Vuai Shein wa shina namba 1 Kadarani Chokocho.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na balozi mstaafu mzee Makame Bakari Haji alipomtembelea nyumbani kwake na kumjulia hali kutokana na kuugua maradhi.

 Baadhi ya vijana wa CCM wakiimba wakati alipokuwa wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kambi yao iliyopo Chokocho wilaya ya Mkoani Kusini Pemba.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiiimba wimbo na vijana hawapo pichani pamoja na viongozi wengine.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa CCM wakati alipozindua darasa la Itikadi katika kambi yao huko Chokocha Kusini Pemba.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Vuai Ali Vuai akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mjimbini wilaya ya Mkoani.

 Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya wana CCM wakiwa mkutanoni.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mjimbini.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment