Monday, 19 January 2015

KINANA AMALIZA ZIARA KATIKA JIMBO LA UZINI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Uzini na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha mapinduzi Mh. Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Dunga wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2010, Katika mikutano mbalimbali ambayo Kinana amekuwa akihutubia na kuzungumza na wananchi na wana CCM amekuwa akihimiza viongozi kufuata maadili ya uongozi jambo ambalo ni muhimu na la lazima katika uongozi ili kuutumikia umma katika misingi mizuri na yenye tija,
Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana wa pili kutoka kushoto akiwa katika mkutano wa ndani pamoja na wawakilishi wenzake wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga. 4 
Ndugu Sauda Mpambalyoto Katibu wa CCM wilaya ya Kati mkoa wa Unguja Kusini akisoma taarifa ya utekelezaji ya chama cha mapinduzi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga leo. 5 
Baadhi ya wana CCM wakifurahia wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika soko la Unguja Ukuuu jimbo la Koani. 10Mwakilishi wa jimbo la Chwaka Mh. Issa Haji Gavu akizunguza wakati alipokabidhi misaada mbalimbali katika jimbo lake la Chwaka. 11 
Injinia Heri Tumaini Mkurugenzi wa kampuni ya CHECOTEC (T) LTD inayojenga barabara katika jimbo la Chwaka akishukuru na kuzungumza maneno yenye hisia ya furaha yake kwa kukutana na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 13 
Mmiliki wa shamba hilo Bw. Ali akizingumza na kumshukuru katibu mkuu wa CC kwa kutembelea shamba hilo. 16 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni jimbo la Uzini. 20 
Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono yao kuashiria kuiunga mkono na kuipitisha Katiba mpya iliyopendekezwa. 21 
Mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib akiwahutubia wananchi wa jimbo la Uzini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni. 22 23 
Baadhi ya wawakilishi wa timu mbalimbali wakiwa na jenzi zao zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib. 24 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.

No comments:

Post a Comment