Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Salmin Awadhi Salmin (pichani) amefariki dunia ghafla mchana huu akiwa mkutanoni katika ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.
Salmin Awadh ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mnadhimu wa wajumbe wa CCM Baraza la Wawakilishi Zanzibar amefariki wakati akihudhuria vikao vya chama.Marehemu Awadh alikimbizwa kwa matibabu Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi zaidi.
Fullahangweblog inatoa pole kwa Wana Magomeni, Familia ya Marehemu, Ndugu jamaa na Marafiki wote na Wazanzibar wote kufuatia msiba huo.
No comments:
Post a Comment