Saturday, 28 March 2015

AFRIKA WALILIA KITI CHA BARAZA LA USALAMA

1
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Vijana viongozi wa Afrika na China wakiwa baadhi ya majarida na mitandao kwenye simu katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Ngurudoto mkoani Arusha kuanzia leo ambao unafunguliwa na Rais wa Zaimbabwe Mzee Robert Mugabe.
2
DSC_7994
Baadhi ya vijana wa kitanzania, wa Kenya na Sudan Khartoum kutoka kulia ni Kokuri Chepkey,Pitia Solomon, Ahmed Farouq Hassan Hamisa Miraji.
………………………………..
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
.
NCHI za bara la Afrika zimeendelea kulilia kiti cha uwakilishi katika
baraza la usalama la umoja wa mataifa ili ziweze kujiwakilisha vyema
katika kuzungumzia matatizo yao kuliko ilivyo sasa ambapo nchi hizo
zinasemewa pasipo uwakilishi wake.
Kilio hicho kilitolewa leo na mwakilishi wa vijana kutoka nchi ya
Niger katika kongamano linalofanyika mkoani Arusha la kzungumzia mambo
mbalimbali zikiwemo fursa za ajira na mengineyo kwa vijana wan chi za
bara la Afrika.
Kufuatia kilio hicho ndipo Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Bernard Membe alipotolea tamko jambo hilo na kuiomba nchi ya
China ambayo ni mwanachama katika baraza hilo na raifiki wa nchi za
Afrika kufikisha kilio hicho kwanchi zingine wanachama.
Membe amesema mchakato wa maombi ya uanachama katika baraza hilo
ulianza muda mrefu lakini kumekuwa na vikwazo mbalimbali kwa nchi za
Afrika jambo ambalo limekuwa likisababisha mikwamo lakini hata hivyo
nchi hizo hazijakata tama na kwamba zinaendelea kuomba.
Amesema awali lilikuwepo ombi la kupatiwa jambo nafasi mbili za
uwakilishi kwa nchi mbili za Afrika lakini bado imeonekana kuwa ngumu
lakini bado wameendelea kuwasilisha maombi hayo japo kwa hata nafasi
moja ili kuweza kusemewa mambo yao sawa sawa.
Ametaja moja ya kikwazo kikubwa kwa nchi hizo za Afrika kuwa ni lazima
ziwe zinatumia nuklia ambapo suala hilo ni gumu kwa nchi hizo za
Afrikalini waliwasilisha ombi la kuruhusiwa kutumia na kutengeneza
nuklia ili kuweza kumudu kuingia katika baraza hilo lakini hadi sasa
maombi hayo hayajajibiwa.
Amesema kinachofanyika kwasasa katika baraza hilo si sawa kwakua
baraza limekuwa likitumia muda mwingi kujadilia masuala ya nchi 54 za
bara la Afrika huku likikosa majibu sahihi kutoka kwa nchi za bara
hilo kutokana na kukosa uwakilishi wan chi hizo.
Amesema zipo taarifa kuwa baraza hilo liliahidi kutoa nafasi hiyo ya
uwakilishi wa nchi za Afrika kuwa mzunguko ili kutoa nafasi kwa nchi
hizo lakini bado hata ahadi hiyo haijatekelezwa hadi sasa pasipo na
maelezo yoyote.
Nchi zingine zilizo wanachama wa baraza hilo lililoanza tangu mwaka
1945 ni pamoja na Urusi,Marekani,Uingereza,Ufaransa na yenyewe China
huku nchi ya Brazili ambayo ilijitahidi kwa nguvu zake zote lakini
haikufanikiwa kuingia katika baraza hilo.

No comments:

Post a Comment