KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,amekanusha
taarifa zilizopo kuwa chama hicho kinakisaidia Chama cha ACT Wazalendo
akidai kuwa hawana sababu ya kufanya hivyo.
Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Nape zinasisitiza
kuwa CCM hakina sababu ya kusaidia chama kingine cha siasa hivyo uvumi
huo ni uchafuzi wa kisiasa.
Akizungumzia kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo(Chadema, Dk Wilbroad Slaa,kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi
imeanza kuandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ngome ya CCM
alisema huo ni upotoshaji uliokubuhu kwani tanzania nzima ni ngome ya
chama hicho.
Alisema ratiba ya NEC haijapangwa kimkakati kama alivyodai
Dk Slaa na kila mtanzania ataandikishwa kwa mujibu wa sheria hivyo kauli
za kuwapotosha na kuwapa hofu wananchi hazina mashiko.
"Kauli hizi za Dk Slaa mzee kama yule ni uthibitisho tosha kwamba wenzetu vyama vya upinzani hasa chadema siasa zao zina lengo la kuwagawa watu kikanda,kanda wanayoiona ni kaskazini, uthibitisho wa mbegu mbaya ya chuki," alisema Nape
Alisema CC"Kauli hizi za Dk Slaa mzee kama yule ni uthibitisho tosha kwamba wenzetu vyama vya upinzani hasa chadema siasa zao zina lengo la kuwagawa watu kikanda,kanda wanayoiona ni kaskazini, uthibitisho wa mbegu mbaya ya chuki," alisema Nape
M wanalaani vikali siasa za namna hiyo kwani
hizo sio hoja za msingi ila ni za kuwagawa wananchi na kupandikiza chuki
zisizokuwa na maana na suala hilo linaonyesha jinsi wapinzani
wanavyofanya siasa za kikanda.
"Tunayo taarifa kwamba Dk Slaa,Mwenyekiti wa
Chadema,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekiti wa Nccr-Mageuzi,James Mbatia
walikaa vikao wakawatenga wenzao wanaunda Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa,
ambao ni Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba ambaye anatokea
Tabora na DK Emmanuel Makaidi ambaye anatoka Kusini, hao wote tunajua
wanatoka mikoa gani,"alisema Nape
Nape alisema siasa za namna hii zinazigawa nchi na
kinachoonekana ni kwamba wapinzani wanajua kuwa watashindwa na ccm ndio
maana wanatafta sababu,hivyo anawatoa hofu wananchi kuwa kila mtu mwenye
sifaa ataandikishwa.
"Chadema wanajua watawaangusha vibaya, hatuna mpango wa
kutumia mizengwe watanzania watatuchagua, waache kuwagawa watanzania kwa
kutaka madaraka, wanatakiwa kuwashawishi wananchi kujiandikisha kama
CCM tunavyofanya"alisema Nape
"Wanapandikiza mbegu mbaya na chuki yenye lengo la kugawa
watanzania,nchi hii ni moja ina makabila 136 na tunaishi vizuri hizi
siasa chafu hazifai,, maneno ya hovyo ambayo hayastahili kusemwa na mtu
mzima kama yule, watashindwa ndio maana wanasema watu wanaandikishwa
kiujanja ujanja, wameanza kujenga mbinu za ajabu, wananchi wanatupenda
na watazidi kutuchagua,"alisema Nape
Alivitaka vyama vya siasa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na waliache zoezi hilo liende kama lilivyopangwalilivyopangwa, wasiwajengee watu hofu, hii sio sawa.
Alivitaka vyama vya siasa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na waliache zoezi hilo liende kama lilivyopangwalilivyopangwa, wasiwajengee watu hofu, hii sio sawa.

No comments:
Post a Comment