MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema uchaguzi mkuu mwaka huu, lazima chama hicho
kihakikishe kinateua wagombea wanaozika na kukubalika kwa wananchi
kwa ngazi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais huku akitaka chama hicho
kusoma alama za nyakati.
Rais Kikwete amesema hayo leo mjini wakati anafungua kikao cha
Halmashauri Kuu(NEC) ya chama hicho kiliachoanza kikao chake cha siku
mbili leo jioni ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mchakato wa
uchaguzi mkuu.
Amesema kuwa wajumbe wa halmashauri kuu wahakikishe
wanachagua mgombea anayekubalika kwa wananchi huku akiendelea kufafanua kuwa
wana CCM wapo milioni sita lakini watanzania wanaopiga kura ni milioni
23.
“Msipochagua watu wanaokubalika na kuuza kwenye uchaguzi mkuu
mtajikuta mnashindwa hata kuwa chama cha kwanza cha upinzani
kutokana na matokeo mabaya mtakayoyapata,”alisema Rais Kikwete.
amesema CCM itambue kuwa kama wao watapitisha jina la mgombea
kwasababu ya kuogopana , basi wananchi hawatawaogopa na watachagua
mtu kulingana na mahitaji yao.Hivyo CCM mkahakikishe anayechaguliwa
basi anakubalika kwa wananchi.
“Lazima tuwe na wagombea wataakaokubalika kwetu na jamii ya
kitanzania.Tukipeleka mtu ambaye hakubaliki kwa wananchi itakula
kwetu,lazima tutambue alama za nyakati,”alisema.
Rais Kikwete alisema kama CCM wanaogopana , watambue wananchi
hawawaogopi ila lazima pia ifahamike chama kwanza ,mtu baadae.
“Tunajukumu la kutafua wagombea watakaotuletea heshima , pia maslahi
ya chama ni makubwa kuliko ya mtu mmoja mmoja.Hivyo tufanye mambo
kwa misingi tuliyojiwekea,”alisema Kikwete.
Amewakumbusha wana CCM
usemi wa Mwalimu Julius Nyerere kwamba Rais anaweza kutoka chama
chochote lakini Rais bora atatoka CCM.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhaman Kinana alisema
jumla wajumbe wote ni 574 lakini waliokuwepo kwenye kikao cha jana
ilikuwa ni 342 sawa na asilimia 92.
No comments:
Post a Comment