Tuesday, 19 May 2015

RAIS WA MSUMBIJI AAHIDI KUSHIRIKIANA KUENDELEZA CHUO CHA DIPLOMASIA

indexNa Magreth Kinabo – Maelezo
………………………………
 
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi ameahidi kueleleza ushirikiano wa pamoja  katika kukuza na kuendeleza Chuo cha Diplomasia  kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam ili kuweze kuwa chuo  chenye kiwango cha juu  cha Kimataifa.
Kauli hiyo  ilitolewa leo na Rais Nyusi wakati alipotembelea chuo hicho, ambapo alisema katika mazungumzo yake na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete wamezungumzia jinsi ya kukiimarisha ili kiweze kuwa kumbukumbu ya wapigania uhuru si kwa nchi hizo bali hata kwa nchi za Kusini wa Afrika.
“Mimi  na Rais Kikwete katika mazunguzo yetu  ya jana , tumezungumzia jinsi ya kuendeleza kituo hiki .” alisema Rais Nyusi.
Aidha Rais Nyusi aliahidi kutoa nafasi ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo kupitia ushirikiano huo, ambapo wanafunzi wa chuo hicho na wakufunzi watakuwa wanakwenda Msumbiji kwenye .
Aidha  Rais Nyusi aliwataka wanafunzi wa chuo hicho, kujiandaa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza  katika serikalini na   sekta binafsi wakiwa wanadiplomasia  badala ya kutegemea kuwa mabalozi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho, Balozi Mwanahidi Majaar alisema  wanampango wa kukiboresha chuo hicho ili kiweze kuwa chuo bora cha kimataifa katika nchi zilizo Kusini mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment