Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mji wa
Kayanga kwenye uwanja wa Kayanga wilayani Karagwe akiwa katika ziara
yake ya kikazi ya mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza yenye lengo la
kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na
wananchi, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi CCM.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KARAGWE)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa
akizungumzia suala la wakulima wa kahawa mkoani Kagera ambao wamekuwa
wakipunjwa kutokana na bei ndogo ya zao la kahawa ukilinganisha na
Uganda jambo ambalo linatokana na kodi nyingi zilizowekwa kwenye zao la
kahawa nchini Tanzania ambazo zote zinaenda kumuangukia mkulima.
Baadhi
ya wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa Kayanga
wilayani Karagwe.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aukiwasili katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nyaishozi.
Mmoja wa wasanii akipiga ngoma wakati wa mapokezi ya Kinana katika kijiji cha Kaishozi
Wafanyakazi
wa kampuni inayojenga barabara ya Kyaka -Begene wilayani Karagwe
wakiendelea na kazi wakati Kinana alipokagua ujenzi wa barabara hiyo
iliyokamilika kwa asilimia 85%.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa barabara ya Kyaka -Begene wilayani Karagwe.
Mkuu
wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella katikati, Mkuu wa wilaya ya Karagwe
Mh Deodatus Kinawiro kulia na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera mama
Costansia Buhie ni miongoni mwa viongozi wa mkoa wa Kagera
walioambatana na Kinana katika ziara hiyo.
Kinana akisalimiana na Deodatus Kinawiro Mkuu wa wilaya ya Karagwe mara baada ya kuwasili wilayani humo.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akishuka kwenye mtambo
mkubwa wa kisawazisha mashamba ya miwa katika kiwanda cha Kagera Sugar
wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua
utayarishaji wa mashamba hayo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye mtambo mkubwa wa
kisawazisha mashamba ya miwa katika kiwanda cha Kagera Sugar wakati
Katibu Mkuu huyo alipokagua utayarishaji wa mashamba hayo.
Moja ya Mitambo hiyo ukiwa umeegeshwa tayari kwa kazi ya kusawazisha mashamba hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha mtambo mkubwa wa
kisawazisha mashamba ya miwa katika kiwanda cha Kagera Sugar wakati
alipokagua utayarishaji wa mashamba hayo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mtaalam wa kilimo
Bw. Chriss Davis wakati alipokagua utayarishaji wa mashamba ya miwa
katika kiwanda cha Kagera Sugar mkoani Kagera.
Kazi ikiendelea.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wataalam mbalimbali
wa kilimo katika mashamba ya miwa ya kiwanda cha Kagera Sugar mkoani
Kagera.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na uongozi wa kiwanda
cha Kagera Sugar wakati alipokagua mitambo ya kusukuma maji iliyojengwa
kandokando ya mto Kagera ambayo inatumika kumwagilia miwa wa pili kutoka
kushoto ni Nassir Seif Mkurugenzi wa kiwanda hicho na wa pili kutoka
kulia ni Ashwin Rana Meneja Mkuu, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.
John Mongella.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mitambo hiyo jinsi inavyofanya kazi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wataalamu
mbalimbali wanaoendesha mitambo ya kilimo cha umwagiliaji katika
mashamba ya miwa ya kiwanda cha Kagera Sugar, kulia ni Mbunge wa Nkenge
mama Asumpta Mshama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Meneja mkuu wa
Kiwanda cha Kagera Sugar Bw.Ashwin Rana wakati akitembelea kiwanda cha
sukari cha Kagera Sugar kushoto ni John Mongella Mkuu wa mkoa wa Kagera.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mmoja
wa wataalamu wa uzalishaji katika kiwanda cha Kagera Sugar wakati
alipotembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji na changamoto
mbalimbali zinazokabili kiwanda hicho.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Meneja mkuu wa
Kiwanda cha Kagera Sugar Bw.Ashwin Rana wakati akitembelea kiwanda cha
sukari cha Kagera Sugar
Mkuu
wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella akifafanua jambo wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika kiwandani hapo wakati Katibu Mkuu huyo
alipotembelea kiwanda hicho.
Meneja
mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar Bw.Ashwin Rana akiwasilisha mambo
kadhaa wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea
kiwanda cha Kagera Sugar mkoani Kagera.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na wakati na kuelekea
kwenye ukumbi wa mikutano na Bw. Ashwin Rana Meneja Mkuu wa Kiwanda cha
Sukari Kagera Sugar.
No comments:
Post a Comment