Na Kipimo Abdallah
JUMUIYA
ya Vijana ya Chama Cha Wananchi (JUVICUF) imewataka vijana wa chama
hicho kujitokeza kugombea katika chaguzi za vijana pamoja na ule wa
Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini kote.
Rai
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa (JUVICUF) Hamidu Bobali wakati
akizungumza na mwandishi wa habari katika ofisi za chama cha CUF jijini
Dar es Salaam.
Alisema
chama kupitia (JUVICUF) kinatarajia kufanya chaguzi kuanzia matawi,
kata, wilaya na Taifa ambapo wilaya 45 za Tanzania Bara na 10 za
Zanzibar zitashiriki ili kupatikana kwa viongozi.
Bobali
alisema mikakati (JUVICUF) ni kuhakikisha kuwa chama kinajijenga vizuri
kuanzia ngazi za chini hasa ukizingatia kuwa ni wakati wa uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu.
“Napenda
kutumia nafasi hii kuwahimiza vijana wa CUF kujitokeza katika chaguzi
zote za chama katika ngazi ya vijana ambazo zimeanza kufanyika sasa na
mwezi ujao Novemba ili mwezi Desemba tuweze kufanya uchaguzi mkuu wa
vijana Taifa”, alisema.
Bobali
alisema uchaguzi huo wa Taifa unatarajiwa kuhusisha zaidi ya vijana 135
kutoka Bara na 120 kutoka Zanzibar ambao watotokana na chaguzi katika
ngazi za Wilaya.
Alisema
mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanakuwa na wawakilishi kutoka Wilaya
zote za Tanzania Bara kama ilivyo Zanzibar ambayo italeta ushindani wa
kisiasa hapa nchini.
Naibu
Katibu huyo alisema pia JUVICUF inajipanga kufanya operasheni
mbalimbali ambazo zitakuwa na lengo la kuhamasisha vijana kujitokeza
katika chaguzi na ufahamu juu ya lengo la Wabunge wanaounga mkono Rasimu
ya Jaji Warioba kutoka nje ya Bunge.
Alisema
kuna hali ya sintofahamu kwa baadhi ya vijana na wananchi mbalimbali ya
nini sababu ya wajumbe wa UKAWA kutoka nje ya Bunge hivyo JUVICUF
inaona ni wakati muafaka wa kutoa elimu.
Bobali
alisema ni vema vijana wa vyama vinavyounga mkono UKAWA kuendelea kuwa
na umoja ili kuhakikisha kuwa juhudi za viongozi wao wa Kitaifa
zinafikiwa ili waweze kukomboa Taifa.

No comments:
Post a Comment