Sunday, 14 September 2014

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA KATIBU MKUU WA CCM AENDELEA NA ZIARA RUFIJI

Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Juma Abeid Diwani wa Kata ya Magawa wilayani Mkuranga wakati alipotembelea shamba la Mikorosho lenye hekari 1000 ambapo mikorosho inayokaribia elfu 20 imeharibika vibaya baada ya kupata ugonjwa unaonyausha mikorosho hiyo , Diwani huyo amesema wananchi wa kata hiyo wako katika hali mbaya kwakuwa zaidi ya miaka minne sasa hawajavuna chochote na maisha yao yanazidi kuwa mabaya, Katibu Mkuu Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- 2 
Mmoja wa wapiga ngoma wa kikundi cha ngoma cha mjini Utete akipiga ngoma huku akiwa amebeba mtoto wake mdogo na mtoto wake mwingine akiwa amekaa pembeni. 15 
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo. 17 
Mkuu wa wilaya ya Rufiji Mh. Nurdin Babu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Utete leo 18 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Utete wakati wa mkutano wa hadhara uliofnyika mjini Utete.  21 
Baadhi ya wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama 23 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dr. Onesmo Mambosho Mganga Mfawidhiwa wa kituo cha afya cha Nyamwage.

No comments:

Post a Comment