Mjumbewa Bunge Maalum la KatibaambayepianiMwenyekitiwaVyamavyaSiasavinavyounda TCD, Mhe. John Cheyo.
(Pichana Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba
ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD Mhe. John Cheyo amewataka Watanzania
kutodanganywa kuhusiana na mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe.
Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha asubuhi
cha Jambo kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Habari Tanzania
(TBC).
Mhe. Cheyo amesema kuwa ni vema
viongozi kuacha kusema uwogo na kuwa waungwana katika mchakato wa
kutafuta Katiba Mpya kwani si vema kuitakia Tanzania mabaya bali ni
kutaka mchakato huo wa Katiba uendelee kwa amani.
Ameongeza kuwa Taifa la Tanzania
linahitaji kuwa Taifa lenye nguvu kwani amani haiwezu kuwekewa thamani
kwa vurugu, hivyo ametaka amani iliyopo nchini ilindwe na kuepuka
kudanganywa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na nchi.
Mhe. Cheyo ameshangazwa kwa
kitendo cha viongozi wa UKAWA kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge
hilo wala kuzungumzia kuhusu suala hilo la kurudi ndani, bali wamekuwa
wakitaka wajumbe wengine walioko ndani watoke kwa kusema kuwa bunge hilo
sio halali.
“Nawashangaa UKAWA kwa kutoweka
ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hili Maalum la Katiba na badala yake wao
wanaweka ajenda ya kutoka ndani ya bunge hili tena kwa nguvu”, alisema
Mhe. Cheyo.
Aidha, Mhe. Cheyo amewataka
vijana nchini wawe na mshikamano na kuepuka kudanganywa na viongozi kwa
kuambiwa mambo yenye uwongo huku akisisitiza kuwa Rais aliyeko sasa hivi
ana nia njema ya kuipatia nchi Katiba iliyo bora na yenye kumfaa kila
Mtanzania.
“Vijana achene kuvunjika miguu
yenu bure, achene kukimbia kimbia barabarani huku mkilishwa maneno yenye
uongo kuhusiana na mchakato huu wa Katiba, vunjikeni miguu kwa kufanya
kazi kwa bidiii na sio kusikiliza uwongo”, alisema Mhe. Cheyo.
Akizungumzia kuhusu TCD, Mhe.
Cheyo amefafanua kuwa TCD ni Jukwaa la majadiliano kwa ajili ya
maridhiano na mapatano pale panapokuwa na tofauti kati ya vyama vya
siasa.
“TCD ni Jukwaa kwa ajili ya
kufanya majadiliano na si vinginevyo, hii ni meza ya maridhiano na
nawaambia kuwa huko mnapokwenda ni kuchepuka, rudini ndani kwenye njia
kuu”, alisisitiza Mhe. Cheyo.
Naye mjumbe wa Kamati namba Sita
ya Bunge Malaam la Katiba Mhe. Steven Wasira amewaasa Watanzania kwa
kusema kuwa, watu wanaosema kuwa Bunge limenyofoa baadhi ya mambo muhimu
yanayohusu wananchi ni waongo na wenye nia ya kupotosha Umma wa
Tanzania.
“Kuna watu wanasema kuwa Bunge
Maalum la Katiba limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi
huo ni uwongo, ni mambo gani hayo yaliyonyofolewa? kwasababu kuna mambo
mengi yameongezwa na kuboreshwa katika mapendekezo kwa ajili ya makundi
mbalimbali ndani ya hiyo Rasimu”, alisema Mhe. Wasira.
Mhe. Wasira ameongeza kuwa
katika Bunge hilo kuna Ibara ya Rasimu ya Katiba na sio ibara za CCM,
amewataka Watanzania nchini wafanya uchunguzi na kusikiliza kwa
kuchambua ili kupata ukweli wa hayo.
“Sisi tuko tayari kuvaana na
viopngozi wowote kwani tunataka Watanzania wote waamini shughuli
zifanywazo ndani ya bunge hili na waepuke kudanganywa”, alisema Mhe.
Wasira.
No comments:
Post a Comment