Wananchi watakiwa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura
KILIMANJARO
wananchi katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wametakiwa
kujitokeza kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwenye uchaguzi
wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba 14 mwaka huu.
Wito
huo ulitolewa jana na Msimamizi mkuu wa uchaguzi katika Manispaa ya
Moshi, Shaaban Ntarambe, wakati akizungumza na waandishi wa habari jana
ofisini kwake mjini Moshi.
Alisema
wakazi wote katika manispaa ya Moshi wanawajibu wa kujitokeza kwa wingi
kwenye zoezi la kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali
za mitaa ili kuweza kutimiza haki ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua
viongozi wanaofaa.
Aidha
alisema zoezi la uandikishaji wapiga kura linatarajiwa kuanza Novemba
23 mwaka huu na kumalizika Novemaba 29 mwaka huu na kwamba vituo
vitafunguliwa saa 1:30 na kufungwa saa 10:00 jioni.
Aliongeza
kuwa zaidi ya vituo 102 vitatumika katika zoezi hilo kwenye kata zote
21 na mitaa yote katika manispaa ya Moshi na kwamba halmashauri hiyo
imejipanga vizuri kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
Katika
hatua nyingine Ntarambe alisema ulinzi wa wananchi umeimarishwa katika
vituo hivyo na kwamba wananchi wasiogope kujitokeza kwa kuhofia hali ya
ulinzi na usalama wao.
No comments:
Post a Comment