Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akitoa salaam za
pongezi kwa wananchi wa kijiji cha Kilangala B kata ya Kilangala kwa
kuipa ushindi CCM kwenye uchaguzi serikaliza mitaa uliofanyika desemba
2014, Katika mkutano huo Nape aliwaeleza wananchi hao CCM ndio chama
pekee kinachotoa majibu kwa matatizo ya wananchi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti aliyeshinda
uchaguzi Hamid Rashid Namtonda akitoa salaam za kushukuru wakazi wa
kijiji cha Kilangala B kata ya Kilangala jimbo la Mchinga.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Kilangala B akiwashukuru wananchi wake kwa kumchagua
kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ,vijiji na vitongoji uliofanyika
desemba 2014.
Mbunge
wa Jimbo la Mchinga Mheshimiwa Said Mtanda akiwahutubia wananchi wa
kijiji cha Kilangala B wakati wa kumtano wa kuwashukuru na kuwapongeza
wananchi wa kijiji hicho kuichagua CCM, mkutano huu ulifanyika tarehe 11
Januari 2015.
Wananchi wakisikiliza salaam za shukrani kutoka kwa Viongozi wao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Lindi.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Bernard Membe
akiwasalimu wajumbe waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa
wa Lindi.
MNEC
wa Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete akishauriana jambo na Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza wakati wa kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Lindi
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Lindi.









No comments:
Post a Comment