Friday, 23 January 2015

KINANA APOKELEWA KWA MCHAKAMCHAKA WA NGUVU JIMBO LA DONGE

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka kushoto  akipokelewa kwa mchakamchaka na Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu  Sadifa Juma Khamis wa tatu kutoka kushoto pamoja na vijana wa jimbo hilo ambao walikimbia naye umbali wa kilomita moja wakiwa katika mapokezi hayo yaliyotia fora mara baada ya kuanza ziara yake katika jimbo hilo leo akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DONGE-KASKAZINI UNGUJA B)2 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza jambo mara baada ya  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushiriki ujezni wa ofisi ya CCM tawi la Muembe Jogoo.15 
Baadhi ya wanafunzi wa madarasa ya Amali  huko Kinduni jimbo la Kitope wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati alipokagua na kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya katika masomo yao .16 
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Maskani ya CCM Kizota jombo la Kitope.22 
Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.23 
Balozi Ali Karume akitema cheche zake kuhusu Katiba Mpya iliyopendekezwa na kuwashawishi wananchi waipigia kura ya ndiyo.24 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.2526 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika Maskani ya CCM Kizota.27 
Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Idd akiwahutubia wananchi wa jimbo la Kitope Kaskazini Unguja.28 

No comments:

Post a Comment