Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kushota), akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Business Times, Imma Mbuguni, alipowasili katika Ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, akiwa katika mwendelezo wa ziara ya vyombo vya habari aliyoianza wiki iliyopita
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Busness Times, Imma Mbuguni (kulia) akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye aliyetembelea ofisi za Business Times jijini Dar es Salaam.
Meneja Usambazaji wa Kampuni ya Business Times Sophie Mshangama akiuliza swali kwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliyetembelea kampuni hiyo inayochapa gazeti la Majira, Business Times na Sports Starehe.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kulia) akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Business Times, Wachapichaji wa Magazeti ya Majira, Business Times na Sports Starehe.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kulia) akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Business Times, Wachapichaji wa Magazeti ya Majira, Business Times na Spoti Starehe, akiwa katika mwendelezo wa ziara ya vyombo vya habari aliyoaianza wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.
Mhariri wa gazeti la Spoti Starehe Charles Mateso akiuliza swali linalohusu namna wasanii wanavyotumika kwenye shughuli za siasa kwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye aliyetembelea leo kwenye kampuni ya Business Times na Business Printer LTD
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa mkutano na wahariri wa magazeti ya Majira, Spoti Starehe na Business Times ikiwa sehemu ya ziara yake kwenye vyombo vya habari yenye lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano, wengine pichani ni Mhariri Mkuu wa gazeti la Majira Ndugu Eckland Mwaffisi (katikati) na Mhariri Mtendaji Imma Mbuguni (kulia)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimuonyesha kalenda ya CCM 2015 Mhariri Mtendaji Imma Mbuguni wa kampuni ya Business Times mara baada ya kumaliza mkutano na wahariri wa magazeti yaliyochini ya Business Times.








No comments:
Post a Comment