Saturday, 21 March 2015

LOWASSA: MASHEKHE WA BAGAMOYO MMENISHAWISHI KUGOMBEA URAIS 2015

 Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiwa amepokea fedha zilizo changwa na Mashekhe kutoka Wilaya ya Bagamoyo. Walio mkabidhi fedha hizo ni Shekhe Yusuf Surul (kulia) na Ally Mtumwa. Mwingine ni Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya.
MASHEIKH wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania urais 2015. Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.
 MASHEKHE hao wakiwasili nyumbani hapo kwaajili ya mazungumzo na Lowassa.
 Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasikiliza viongozi wa msafara huo.
 Edward Lowassa akizungumza na Mashekhe hao mjini Dodoma.
 Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlingotini, Kaole, Chalinze, Lugoba, Msata na kwingineko.
 Duaa ilisomwa na viongozi hao wa dini.
  Edward Lowassa akiwasindikiza viongozi hao.
 Lowassa akiagana na Sheikh Alli Mtumwa mmoja wa viongozi wa msafara huo.
 Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiagana na viongozi hao.
 Lowassa akimsikiliza mmoja wa Mashekhe hao.

No comments:

Post a Comment