…………………………………………………………….
Na Abou Shatry Washington DC
Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe wa chama cha wananchi CUF Mhe: Ismail Jussa Ladhu amesema Tanzania inaelekea kusipotarajiwa na maoni waliyotoa wananchi kwa ajili ya Bunge la Katiba.
Aidha amesema matarajio ya watanzania hayajatimizwa mbali ya kuwepo mijadala mingi juu ya rasimu ya Jaji Warioba ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu Suala la katiba mpya.
Mhe. Jussa aliyasema hayo wakati akizungumza na Watanzania wa DMV siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall 1401 University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
Pia Mhe. Jussa ambaye pia ni mjumbe wa UKAWA amesema uamuzi wa UKAWA kususia na kujitoa katika bunge la katiba ni kwa sababu chama tawala CCM kimekwenda kutetea sera zake na kupinga mawazo ya wananchi ambayo yamewakilishwa katika rasimu ya Jaji Warioba.
Mkutano huo ulijumuisha Agenda kadhaaha ikiwemo Mchakato wa Katiba mpya, Ufafanuzi juu ya muundo wa serikali tatu, Uamuzi wa UKAWA kususia mchakato huo dhalimu na sababu ya maoni ya watu walio Diaspora kuhusu Uraia Pacha kutokutekelezwa kama walivyotarajia.

No comments:
Post a Comment