Sunday, 12 July 2015

UKAWA KATIKA FUTARI, WAKATI WA KIKAO CHA MIKAKATI

uk1
 Baadhi ya Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutoka kushoto, Naomi Kaihula (Viti Maalum CHADEMA), Salum Baruan (CUF- Lindi Mjini) na Mohamed Habib Mnyaa wakishiriki futari iliyoandaliwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA (Summit) kilichojadili mikakati mbalimbali ya maandalizi ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
uk2
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini),Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni) na Mama Riziki.
uk3
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Vioingozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini) na Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni).
uk4
Baadhi ya Wabunge na Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) wakiwa katika futari ya pamoja iliyoandaliwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA (Summit).kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
uk5
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa akishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Kushoto kwake ni Mbunge wa CUF, Ali Khamis Seif (Mkoani) na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa NLD Zanzibar, Ahmad Hemed. 
uk6
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed (katikati) pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy (kushoto) huku wakishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.

No comments:

Post a Comment