Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wajumbe baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, leo katika Ukumbi wa jengo la White House mjini Dodoma. Kikao hicho ni cha kuchagua wagombea watatu kati ya watano waliopitishwa na Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya kuwania kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Watatu watakaopatikana leo, watapelekwa kuigiwa kura katika Mkutano Mkuu wa CCM ili kupata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo mkuu. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete kufungua mkutano huo. Kushoto ni Dk. Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kushoto_ alipoingia ukumbini. Waliosimama mbele ni Wajumbe waalikwa wa kikao hicho kutoka Baraza la Ushauri la Wazee Marais wastaafu Ali Hassani Mwinyi na Benjamin William Mkapa na wengine ni Makamu Wenyeviti wastaafu Mzee John Malecela na Mzee Pius Msekwa
Kikao hicho kikiendelea
YALIYOJIRI KABLA YA KIKAO HICHO
Aliyekuwa muomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameenguliwa, Edward Lowassa akiwasili kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM kuhudhuria kikao cha NEC.
Lowassa akiingia ukumbini
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Mzee Msidai akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho cha NEC
Mjumbe wa NEC, Dk. Chegeni akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, wa CCM, Zakiah Megji akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
No comments:
Post a Comment