Tuesday 4 August 2015

MKUTANO MKUU WA CHADEMA WAMPITISHA BILA KUPINGWA MH. LOWASSA KUWA MGOMBEA URAIS WA TANZANIA NA DKT. JUMA HAJI DUNI MGOMBEA MWENZA

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (wa nne kulia) akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa Urais alieteuliwa na chama hicho, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) pamoja na Mgombea Mwenza wake, Mh. Dkt. Juma Haji Duni (mwenye suti nyeusi) pamoja na wanachama wapya wa Chama hicho, wakati wakitambulishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.(PICHA KWA HISANI YA MICHUZIBLOG)
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akizungumza katika mkutano huo.
Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia.
Mgombea Mwenza wa kupitia Chadema Juma Haji Duni akizungumza katika mkutano huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Ndugu Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika mkutano huo
Mgombea Urais kupitia Chadema Ndugu Edward Lowassa akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema mara baada ya kumpitisha kugombea kwa vyama vua UKAWA.


No comments:

Post a Comment