Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafuasi wa chama hicho waliojitokeza katika makao makuu yao yaliyopo Buguruni jijini Dar es salaam na kuwaambia CUF ni Taasisi hivyo wanachama wote wanatakiwa kukijenga chama hicho wawe na vyeo ama wasiwe na vyeo kazi kubwa ni kukijenga chama cha CUF amesema maneno hayo bila kufafanua.
Profesa Lipumba alitakiwakuzungumza na waandishi wa habari katika makao makuu hayo lakini mpaka dakika za mwisho hakufanya mkutano huo badala yake alikuwa na kikao na wazee wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa dini na wanachama na wakati akiondoka katika ofisi hizo ndipo akazungumza maneno hayo hakuyafafanua zaidi.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari katika makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam
Baadhi ya wanachama wa chama cha CUF wakiwa katika makao makuu ya chama hicho wakipiga kelele kuashiria kumuunga mkono mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba.
Wana CUF wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika makao makuu ya chama hicho Buguruni kumsikiliza Mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba
Mpiga Picha wa Gazeti la Uhuru Emmanuel Ndege akisaidiwa na waandishi wenzake mara baada ya kujeruhiwa na feni wakati waandishi hao wakisubiri Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba kuzungumza nao katika makao makuu ya chama hicho Buguruni.
No comments:
Post a Comment