Wednesday 5 August 2015

PROFESA IBRAHIM LIPUMBA NA MINONG'ONO YA KUJIUZULU

IMG_4498
HALI ya kutatanisha juu ya uongozi wa juu wa Chama cha (CUF), imeendelea kuwepo baada ya mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba kutoweka wazi msimamo wake kutokana na taarifa za kutaka kujiuzulu wadhifa wake zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Leo Profesa Lipumba, alipanga kuzungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam, lakini wazee wa chama walimzuia kufanya hivyo hadi atakapowaeleza anawaambia nini waandishi wa habari.
Naibu Katibu Mkuu CUF Bara, Magdalena Sakaya hata yeye hakuwa na taarifa za mkubwa wake (Profesa Ibrahim Lipumba) kuzungumza na vyombo vya habari.
Sakaya alizungumza na waandishi wa habari na kuwaambia
“Tunawaomba radhi mwenyekiti alitaka kuzungumza nanyi mapema lakini kabla hajafanya hivyo alivamiwa na wazee ofisini kwake wakitaka kujua anakuja kusema nini, hivyo mkutano hautakuwepo.
Baadhi ya wanachama wanaopinga Profesa Ibrahim Lipumba kukubali kuwepo ndani ya Ukawa wametishia kuchana kadi zao ikiwa mawazo yao yatapuuzwa.
Baada ya muda Profesa Ibrahim Lipumba alitoka ofisini huku akiwa amezungukwa na walinzi wa chama waliotawanya wanachama waliotaka kumshika mwenyekiti wao, hata hivyo hakuzungumza kwa muda mrefu bali alisema maneno machache na kuondoka huku akiacha minong'ono.
Amesema Chama ni taasisi si mali ya mtu mmoja, ni wajibu wa kila mwanachama kikujenga hata kama si kiongozi amemaliza Profesa Lipumba na kuondoka zake

No comments:

Post a Comment