Monday, 10 August 2015

CCM MTWARA WAUNGANA KUMHAKIKISHIA USHINDI MAGUFULI

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimia wanachama wa CCM mkoa wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumsalimia kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mtwara.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wana CCM wa mkoa wa Mtwara nje ya ofisi za CCM mkoa.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wana CCM wa mkoa wa Mtwara nje ya Ofisi ya CCM mkoa na kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuimarisha Chama.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mtwara ambapo alifika kusalimia na kusaini vitabu vya wageni.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mwigulu Nchemba.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana an Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego akizungumza wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsalimu Mgombea Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli aliyefika ofisini hapo kutoa shukrani kwa wadhamini 231 waliomdhamini kwenye nafasi ya Urais mkoa wa Mtwara ikiwa sehemu ya kutimiza taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Mtwara na kuwaambia Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli atashinda mapema mno.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa Mtwara  ambapo alihakikisha kuwa Mtwara itaongoza katika kumpigia kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Husnain Murji akiwahutubia wana CCM nje ya ofisi ya CCM Mtwara na kuwaambia kuwa ushindi kwa CCM utakuwa wa kishindo .

TAARIFA KWA UMMA, TAARIFA ZA UZUSHI ZILIZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU DKT. BILAL SI ZA KWELI


ngao
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo kwa taarifa za uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Habari hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
10/8/2015

KIMBISA AMKARIBISHA RAIS KIKWETE DODOMA

unnamed (66)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma.Ndugu kimbisa alikanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana   (Picha na Freddy Maro)
unnamed (67)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma. Katikati ni Ndugu kimbisa alikanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni   (Picha na Freddy Maro)
unnamed (68)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma leo

LOWASA ACHUKUA FOMU ZA URAIS

Mgombea wa Nafasi ya Urais Kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akikabidhiwa fomu za Urais na Ofisa wa tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, hii leo alipofika kwenye Ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya Umati wa wafuasi wa Chadema uliofika kwenye Ofisi za Tume ya
Uchaguzi ili Kumsindikiza Mgombea wa Nafasi ya Urais kupitia CHADEMA,
Edward Lowassa hii leo.
 
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu nae alikuwepo kumsindikiza Edward Lowassa kuchukua fomu ya Urais kupitia CHADEMA.

Sunday, 9 August 2015

UONGOZI WA CCM ARUSHA,NANGOLE NA KADOGOO WATIMUKIA CHADEMA

kadogooo11111
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo  Ole Nangole kulia akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kuhamia rasmi chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kushoto niKatibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Isaac Joseph Maarufu kama Kadogoo(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

RAIS KIKWETE AZINDUZA KIVUKO CHA MV MAFANIKO NA KUZINDUA MRADI WA NYUMBA ZA NHC MKOANI MTWARA LEO

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu
akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe
la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa  na
NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia
ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana.
 Sehemu kivuko hicho kilichozinduliwa Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mkoani Mtwara.
 Naibu
Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi
Mh.John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha Mv Mafanikio
mkoani Mtwara mapema leo mchana
 Waziri
wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Jakaya
Kikwete kabla ya uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara
mapema leo mchana,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Fatma Salum Ali.
 Rais
Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Fedha,Mh
Mwigulu Nchemba ambaye pia alihudhuria sherehe hizo fupi uzinduzi wa
kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana
 Rais
Kikwete akizindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio kwenye pwani ya mji wa
Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu
mkoani Mtwara.
  Rais Dkt.Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko cha Mv Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.Kivuko cha MV Mafanikio kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 3.3

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa ameambatana Waziri wa Ujenzi Dkt John
Pombe Magufuli mara baada kushuka kwenye kivuko cha Mv Mafanikio katika
kata ya Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini mara baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya
Kikwete,kivuko hicho kina uwezo wa
kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 3.3
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini waliofika kwenye uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa
kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 3.3
 Baadhi ya wananchi wa Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini wakishangilia jambo mara baada ya kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa
kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 3.3 kuzinduliwa na Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mchana mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akizungumza
jambo mbele ya wananchi wa Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini baada ya uzinduzi wa  kivuko cha MV Mafanikio
chenye uwezo wa
kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 3.3,Dkt Magufuli amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete katika utawala
wake ndani ya maiaka kumi amefanikiwa kujenga vivuko vipya 15 na
vingine 7 vimekwishakarabatiwa na vinafanya kazi mpaka sasa
 Rais
Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini kuzindua kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa
kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 3.3
 Bango la mradi huo
 Mkuruegenzi
Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi Rais
Dkt Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na
wananchi kwa ujumla katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi
zinazojengwa  na
NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,
 Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi  katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na
NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu
pamoja na Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt
John
Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo.
PICHA NA MICHUZI JR-MTWARA